AFYA YA AKILI
Afya ya akili:-Ni ustawi wa mtu pale anapoweza kutambua uwezo wake na kutatua changamoto kufanya kazi na kuchangia katika jamii yake
Afya ya akili si kutokuwa na magonjwa ya akili, sio kua vizuri kiuchumi,sio kutokuwa na akili,afya ya akili ni muhimu kama ilivyo afya ya mwili
DHANA YA AFYA YA AKILI
Afya ya akili inahusu ustawi wa mtu katika ngazi kuu tatu
.ustawi wa jamii
.Akil na fikra
.mihemko na hisia
Afya ya akili inahusu mtu anavyofikiri,mtu anavyote hisi na anavyotenda
Afya ya akili ni ile ambayo inamuwezesha mtu:- .kujitambua kuhusu kipaji na hata udhaifu wako
.Kujifunza kufanya unachopenda na usichopenda
.Kudhibiti na kuhimili changamoto za kimaisha
.kufanya shughuli zake za kimaisha na kuchangia katika jamii yake, familia na taifa kwa ujumla
MAAANA YA UGONJWA WA AKILINi ule ambao humfanya mtu kuwa na hisia,fikra na matendo tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii,kushindwa kukubaliana na changamoto za kimaisha, kushindwa kwajibika pamoja na jamii
AINA YA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI
I.Yasiyoleta kuchanganyikiwa(non-psychotic)
ii.Yanayoleta kuchanganyikiws(psychotic)
INAKUAJE MTU ANAPATA UGONJWA WA AFYA YA AKILI
Visababishi:-
i.matatizo ya kibaiolojia
ii.matatizo ya kisaikolojia
iii.matatizo ya kijamii
**Matatizo ya kibailojia
-kurithi
-Ajali inayohusisha kichwa.
-magonjwa ya ndani mfano (pressure,kaswende, kisukari)
-uharibifu wa ubongo kipindi cha kuzaliwa
**Matatizo ya kisaikolojia
-manyanyaso ya kimwili.
-uwezo mdgo wa kuwasiliana na wengine.
-kutojali watoto.
-kukosa upendo na msaaada wa kutosha kutoka kwa wazazi/walezi
**Matatizo ya kijamii
-kupoteza wazazi kwa umri mdgo.
-kifo cha mtu wa karibu .
-kufirisika.
-umasikini na madeni .
-kuvunjika kwa ndoa.
DALILI ZA UGONJWA WA AKILI
Dalili Za awali
-mabadiliko ya kitabia (kujitenga,ukali,dini kupitiliza)
-mabadiliko katika kula.
-wasiwasi uliopitiliza
-matumizi mabovu ya vilevi
Dalili za baaadae
-kuona au kusikia vitu ambavyo ki uhalisia having
-kuwa na mawazo hasi
-kuwa na fikra danganyifu.
-kuongea mwenyewe au kutokuongea kabisa
-
UNATAMBUAJE KUWA UNA TATIZO LA UGONJWA WA AKILI?
Si rahisi kujitambua
Zifuatazo ni baaadhi tu ya dalili za kujitambua
*kutopendelea sana au kuwa na furaha kidogo wakati unafanya jambo
*kupata mfadhaiko ,huzuni au kuishiwa matumaini
*kupata usingizi kwa shida au kulala sana au kulala muda mfupi
*kutokuwa na hamu ya kula au kulankupita kiasi
*kupata hisia mbaya kuhusu wewe,au kufikiria wewe ni wa kushindwa au familia umeiangusha chini
*kushindwa kungalia vitu kama vile runinga au kusoma gazeti.
*Kuongea taratbu kupita kiasi,hadi watu wengine kuona kinyume chake/ kuhangaika au kutotulia mpaka kuzunguka sehem mara moja isiyo kawaida
*mawazo ya kwamba ni bora kufa au ya kutaka kujidhuru kwa namna yoyote ile
JINSI YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI
-kuijua afya ya akili(mental health awareness)
-kujali afya yako.
-kula vyakula vyenye virutubisho
-kufanya mazoezi
-kufanya vitu unavopenda(hobi)
-kuwa na muda
-usingizi wa kutosha
-kueleza changamoto unazozipitia kwa watu wako wa karibu au msaikolojia au daktari ili kuweza kuondoka na msongo wa mawazo
Swali ni kweli kwamba asilimia kubwa ya matatizo ya afya ya akili yanawakumbuka vijana ?
Zingatia "hakuna afya bila afya ya akili "
Ni kweli hakuna afya bila afya ya akili ,nimeshuhudia rafiki zangu wakijiua, kisa tatizo hili la kukosa elimu juu ya afya ya akiliππ please share your thoughts
ReplyDeleteOyaaa
DeleteNiajeee
DeleteAfya ya akili inaanza na mimi wewe na yule....afya ni afya ya akili
ReplyDeleteContent bomba sana
ReplyDeleteπͺπͺπͺ
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteNiajeeee
ReplyDelete